Muziki

30 ya Bongo Fleva kituo kinachofuata ni Dodoma

DODOMA: KAMATI ya Maandalizi ya Sherehe za Miaka 30 ya Bongo Flava imetangaza kuwa Dodoma ndiyo itakuwa kituo kinachofuata cha maadhimisho hayo, baada ya sherehe hizo kufanyika kwa mafanikio jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa niaba ya Kamati na Hamadi Ally ‘Madee’, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 22, 2026, katika Chinangali Park, Dodoma.

Kamati imetoa shukrani kwa washiriki pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha maadhimisho yaliyofanyika jijini Mwanza, ikieleza kuwa sherehe hizo hazilengi kutoa burudani pekee, bali pia kuwawezesha wasanii na jamii kiuchumi, sambamba na kuimarisha sekta ya uchumi wa ubunifu nchini.

Aidha, Kamati imesema maadhimisho hayo yanalenga kuendelea kuuenzi, kuutangaza na kuimarisha urithi wa muziki wa Bongo Flava, huku safari ya maadhimisho hayo ikiendelea katika mikoa mbalimbali nchini.

Hatua hiyo inatarajiwa kuendelea kuwakutanisha wasanii, wadau wa muziki na mashabiki katika kusherehekea safari ya miaka 30 ya muziki wa Bongo Flava na mchango wake katika sekta ya ubunifu nchini.

Related Articles

Back to top button