LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Dar es Salaam na Tanga.
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga utakuwa shuhuda wa mchezo kati ya wenyeji Coastal Union inayoshika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi ikiw ana pointi 23 baada ya michezo 16 dhidi ya Mtibwa Sugar inayoshika mikia nafasi ya 16 baada ya michezo 15.
Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu timu hizo kukutana Agosti 20, 2023 zilitoka sare ya bao 1-1 mkoani Morogoro.
Namungo ya mkoani Lindi inayoshika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 16 itakuwa mgeni wa KMC iliyopo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 22 kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 zilipokutana katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Agosti 19, 2023 mkoani Lindi.