
DAR ES SALAAM: MUIGIZAJI wa filamu nchini Tanzania, Blandina Chagula maarufu kama Johari, amesema kwa sasa bado yupo single na hajapata mwanaume wa kumuoa.
Akizungumza kuhusu suala la ndoa, Johari amesema yupo tayari kuolewa endapo atajitokeza mwanaume mwenye nia ya kumuoa, huku akifichua kuwa kwa sasa hana vigezo vingi anavyovitazama kwa mwanaume.
Johari amesema katika hatua aliyofikia, anachohitaji ni mwanaume ambaye yupo hai na yuko tayari kuingia naye kwenye ndoa.
“Bado sijapata mtu wa kunioa. Naweza nikasema hivyo, nipo free. Mtu akijitokeza kunioa, nipo tayari.
Kwa sasa nilipofikia, awe tu anapumua,” amesema Johari.




