Ligi Kuu

Fountain Gate ni habari nyingine

KOCHA Mkuu wa Fountain Gate FC, Mohammed Muya ameweka wazi siri ya ushindi katika timu yake ni nidhamu ya wachezaji katika kuheshimu mpinzani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema alipokabidhiwa timu hiyo jambo la kwanza ni kusimamia katika utamaduni wao katika suala la nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Fountain Gate FC wako nafasi ya pili wakicheza mechi tano kushinda tatu, sare moja na wapoteza moja wakivuna pointi 10 za ligi hiyo.

“Ni kweli tumekuwa na ushirikiano na upendo ndani ya benchi la ufundi, kuheshimiana jambo hili tunalipeleka kwa wachezaji wetu katika kazi na kuthamini wanachokipambania,” amesema Muya.

Ameongeza kuwa wanazungumza na wachezaji kwa kufuata utaratibu wao Fountain Gate ambao ni kuheshimiana na inawapa nafasi ya kufanya vizuri katika michezo yao.

Muya amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mapambano kwa kutafuta pointi muhimu katika kila mechi iliyopo mbele yao.

“Tumefanya maandalizi mazuri, tupo nyumbani tinahakikisha tunatumia vizuri uwanja wetu kwa ajili ya kupata matokeo na kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri  katika msimamo,” amesema kocha wa Fountain Gate FC.

Fountain Gate FC wanashuka dimbani kesho wakiwakaribisha Kagera Sugar uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo, Babati.

Related Articles

Back to top button