Ligi KuuNyumbani

Simba mawindoni leo

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba inashuka dimbani leo kuikabili Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikitaka kurejesha makali yake baada ya kupokea kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa watani wake wa jadi Yanga Novemba 5.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 7 wakati namungo ina pointi 7 nafasi ya 12 baada ya michezo 8.

Wakati huo huo nyota wa Simba, Clatous Chota Chama amewaomba wanasimba kuwa kitu kimoja.

Kupitia ukurasa wake wa instagram chama ameandika: “Katika mazingira haya hakuna haja ya kunyoosheana vidole na kubebeshana lawama, haitusaidii chochote. Huu ni wakati sahihi wa kushikamana tukiweka mioyo na mawazo yetu pamoja. Twende tena pamoja ili kujikomboa kutoka kwenye hii hali,” amesema Chama.

Itakumbukwa baada ya Simba kupoteza mchezo mbele ya watani wa jadi Yanga, klabu hiyo ya Msimbazi ilifikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo(Robetinho).

Katika mchezo mmoja wa ligi hiyo uliopigwa Novemba 8, Yanga imevuna pointi 3 muhimu baada ya kuilaza Coastal Union kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 

Related Articles

Back to top button