Ligi Daraja La KwanzaLigi KuuLigi Ya WanawakeNyumbani
Usajili wachezaji kuanza Julai 1

Dirisha la Usajili(FIFA Connect) kwa klabu za Ligi KuuTanzania Bara, Ligi ya Championship(CL), Ligi Daraja la Kwanza(FL) na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara(SLWP) msimu wa 2023/2024 litafunguliwa Julai 1, 2023.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema dirisha hilo la usajili litafungwa Agosti 31, 2023.
“Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, tafadhali zingatia muda huo wa usajili na uhamisho,”imesema TFF.
Aidha shirikisho hilo limesema usajili na uhamisho wa wachezaji kwa dirisha dogo utafunguliwa Desemba 16, 2023 na kufungwa Januari 15, 2024.