Nyumbani

Saido atambulishwa Simba

KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo mshambuliaji aliyekuwa Geita Gold na Yanga Saido Ntibazonkiza baada ya kukamilisha taratibu za usajili.

Akizungumza na SpotiLeo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema Ntibazonkiza amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuwatumikia wekundi wa Msimbazi.

“Ni kweli leo Desemba 24 tumemtambulisha Ntibazonkiza baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wake na zoezi hili bado linaendelea ndani ya siku mbili zijazo tutamtambulisha mchezaji mwingine,” amesema Ahmed.

Ntibazonkiza mwenye umri wa miaka 36 msimu huu tayari amehusika kwenye magoli 10 akiwa na Geita Gold baada ya kutoa pasi za magoli sita na kufunga magoli manne.

Nyota huyo tayari ameshawasili kwenye Kambi ya Simba Jijini Mwanza na huenda akawa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachocheza dhidi ya KMC Disemba 26.

Related Articles

Back to top button