Ligi Kuu

Machi 8 sio mbali Kibu D yupo chimbo

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amefunguka hali ya mshambuliaji wake, Kibu Denis akisema kuwa yupo kwenye mazoezi ya uangalizi akitarajiwa kuwepo mchezo ujao.

Kibu aliumia kwenye mchezo dhidi ya Tabora United na kumfanya kukosa mechi mbili zilizofuata dhidi ya Fountain Gate FC na wajelajela Tanzania Prisons.

Kocha Fadlu amesema Kibu anaendelea vizuri kutokana na matibabu mazuri anayoyapata kutoka kwa madaktari akiwatuliza mashabiki.

“Naweza kusema Kibu anaendelea vizuri chini ya uangalizi, anaendelea kufanya mazoezi. Baada ya ripoti ya madaktari tutaanza kumtumia katika michezo ijayo, mashabiki wasiwe na wasiwasi wowote,” amesema.

Fadlu amesema Simba ina kikosi kipana ndio maana hata akikosekana mchezaji mmoja bado wanaendelea kupata ushindi lengo likiwa ni kuhakikisha msimu huu mashabiki wanapata furaha waliyoikosa kwa misimu kadhaa iliyopita.

“Kibu Denis amekuwa nje ya uwanja kwa michezo miwili hivi lakini bado tuliendelea kupata matokeo mazuri. Hii ndiyo faida ya kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa, niseme tu mapambano yanaendelea,” amesema.

Related Articles

Back to top button