Kikapu

UDSM Outsiders mtaitaka mwaka huu

Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM outsiders imemteua Daud Zablon Maiga kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa muda wote uliobaki wa msimu wa ligi kuu ya mpira wa kikapu, mkoa wa Dar es salaam.

“Tunayo furaha kumpokea kocha @daud_maiga07 ambaye hivi karibuni ameshinda mashindano ya Taifa Cup. Kujitolea,uadilifu na ustadi wake utakuwa nyongeza muhimu kwa timu yetu na shirika kwa ujumla”, imeandika timu hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii.

Sambamba na hilo, timu hiyo oia imemteua Mohamed Mgweno kuwa Mkuu wa utaalamu wa kiufundi katika kutekeleza jukumu la kutathmini utendaji wa kiufundi wa timu na kutoa ushauri wa uongozi kuhusu maeneo yanayohitaji kuboreshwa.

UDSM- Outsiders inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ya mkoa wa Dar es salaam ( BDL) ikiwa imekusanya jumla ya alama 50 ambapo wamecheza michezo 26 hadi sasa, wakishinda michezo 24 na kupoteza michezo miwili. Kinara wa Ligi hiyo ni timu ya Dar City yenye alama 51.

Related Articles

Back to top button