Jesca: Nimepata ajira kupitia michezo

DAR ES SALAAM: MCHEZAJI wa kikapu wa JKT na netiboli Jescar Julius amehimiza vijana wenzake kushiriki michezo kwa kuwa wanaweza kubahatika kama yeye kupata ajira.
Nyota huyo amekuwa miongoni mwa wachezaji wa kike tegemeo wa kikapu kwenye kikosi cha JKT ambaye kwa sasa ameonekana katika timu ya Uhamiaji inayoshiriki michuano ya netiboli.
Akizungumza na gazeti hili nyota huyo amesema watu hawajui hata michezo ni sehemu ya kubahatisha kwa ajili ya ajira hivyo, anawaita vijana wenzake wenye vipaji kujaribu bahati zao.
“Mimi nimeajiriwa kwasababu ya michezo hat ana wengine wanaweza kubahatisha kwa kushiriki michezo tofauti. Unaweza kusoma huku unacheza na ukabahatika,”amesema.
Jesca alianza kucheza kikapu tangu akiwa anasoma Sekondari akawa anashiriki michezo ya vijana kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete hatimaye kipaji kilionekana na baada ya kumaliza masomo ya sekondari akajiunga na wanajeshi.
Sio yeye tu bali wapo vijana wengi wanapata ajira kupitia michezo tofauti sehemu ambako pengine baadhi hawajui kuna fursa.