Kikapu

JKT Stars, Dar City hazikamatiki

DAR ES SALAAM:KLABU ya mpira wa kikapu ya Dar City imeanza vyema mchezo wa robo fainali ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam kwa ushindi wa vikapu 79-45 dhidi ya Srelio katika mchezo wa kwanza uliochezwa jana, oktoba 8 kwenye Uwanja wa Don Bosco, Oysterbay, Dar es Salaam.

Kwa upande wa wanawake, JKT Stars imeshinda mchezo dhidi ya Polisi Stars kwa vikapu 78-53.

Michezo hiyo kwa washindi ni kama wametanguliza mguu mmoja hatua ya nusu fainali,kwani wanahitajika kushinda michezo miwili kati ya mitatu wanayotakiwa kucheza ili kufuzu kwa uhakika.

Dar City na JKT Stars zote ni timu zilizomaliza hatua ya makundi zikiwa vinara na zote zimecheza na waliomaliza nafasi ya nane.

Katika michezo hiyo ya play-offs, wachezaji waliofanya vizuri ni Victor Mwoka wa Dar City aliyefunga pointi 21 na Sara Budodi wa JKT Stars aliyefunga pointi  14.

Timu hizo zitarudiana mchezo wa pili Jumamosi ya wiki hii na matokeo yataamua atakayefuzu nusu fainali.

Michezo mingine itakayochezwa leo usiku ni DB Troncatti dhidi ya Pazi Queens kwa upande wa wanawake na UDSM Outsiders dhidi ya Vijana Basketball Club kwa upande wa wanaume.

Related Articles

Back to top button