EPL

Chelsea yaongoza ada za mawakala

CHELSEA ililipa zaidi ya £75m kwa mawakala wa soka na wasuluhishi katika kipindi cha miezi 12 hadi Februari 2024, huku vilabu vya ‘Premier League’ vikitumia pauni milioni 409.5 kwa jumla.

Gharama ya Manchester City kwenye ada za wakala ilizidi £60m, kulingana na takwimu zilizotolewa na Chama cha Soka zinazoelezea malipo yaliyofanywa na vilabu vya Premier League, EFL na Ligi ya Taifa.

Takwimu hizo pia zinaweza kujumuisha miamala ambayo vilabu viliingia kabla ya kuanza kwa kipindi cha kuripoti Februari 2023.

Chelsea (£75.1m) na Manchester City (£60.6m) waliwazidi mbali wapinzani wao wa Premier League, huku Manchester United wakiwa wa tatu kwa matumizi makubwa (£34m).

Hatua hiyo inakuja baada ya matumizi ya Chelsea katika uhamisho na ada za mkopo tangu Todd Boehly kuchukua umiliki wa klabu hiyo msimu wa joto wa 2022 kuzidi kiwango cha £1bn. Miongoni mwa mikataba hiyo, usajili wa kiungo Moises Caicedo unaweza kupanda hadi kufikia rekodi ya Uingereza ya £115m.

Liverpool (£31.5m), Arsenal (£24.7m) na Aston Villa (£21.1m) zote zilitumia zaidi ya £20m kwa ada ya wakala, huku Tottenham (£19.7m) na Newcastle United (£18.8m) zikiwa nyuma.

Luton Town ilitumia kiwango kidogo zaidi kati ya vilabu vya Premier League, ililipa £2m, kwani klabu zilizoshuka daraja msimu uliopita Leeds United (£13.2m), Leicester City (£8.1m) na Southampton (£7.5m).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button