EPLKwingineko

Everton yanyang’anywa pointi 10

KLABU ya Everton imenyang’anywa pointi kumi baada ya kubainika kukiuka Kanuni za Fedha na Udumishaji (PSR) za Ligi Kuu England.

Adhabu hiyo ni kubwa zaidi ya kimichezo katika historia ya EPL na imeishusha Everton hadi nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi nne.

Afisa Mtendaji Mkuu wa muda wa Everton, Colin Chong amesema klabu imeshtushwa na kusikitishwa na uamuzi usio wa uwiano na haki na kwamba inakusudia kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

“Ukali wa adhabu iliyotolewa sio wa haki wala haulingani na ushahidi uliowasilishwa,” amesema Chong

Machi mwaka huu Ligi Kuu England iliipeleka Everton katika Tume Huru lakini haikufichua vipengele vilivyokiukwa na klabu hiyo.

Katika kipindi hicho Everton ilitangaza hasara ya fedha kwa mwaka wa tano mfululizo baada ya kuripoti upungufu wa pauni milioni 44.7 kwa mwaka 2021-22.

Klabu za Ligi Kuu England zinaruhusiwa kupoteza pauni milioni 105 kwa kipindi cha miaka mitatu na Everton ilikiri kukiuka kanuni hizo za fedha kwa kipindi kinachoishia 2021-22.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button