EPLKwingineko

Willian akaribia kurejea EPL

KIUNGO wa zamani wa Brazil, Willian Borges da Silva, maarufu Willian anakaribia kurejea Ligi Kuu ya Uingereza(EPL) akichezea Fulham.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Arsenal alikuwa akiichezea Corinthians ya Brazil.

Hata hivyo, mkataba wa Willian mwenye umri wa miaka 34 ulifutwa baada ya nyota huyo kudai yeye na familia yake walitishiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii.

Anatarajiwa kufanya vipimo Klabu ya Fulahm na huenda dili likafikiwa baada ya dirisha la usajili kufungwa kutokana na hali ya mkataba wake.

Willian alishinda mataji matano yakiwemo mawili ya Ligi Kuu wakati akiwa Chelsea kwa miaka saba kabla ya kuhamia Arsenal mwaka 2020 kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mkataba wake kwa washika bunduki wa London ulivunjwa baada ya mwaka mmoja kwa sababu hakuwa katika kiwango bora na alihamia katika klabu aliyoanza mpira wa kulipwa ya Corinthians alikozaliwa.

Willian alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Brazil baada ya kuanza kucheza timu ya taifa mwaka 2011 lakini alicheza mchezo wa nwisho wa Brazil mwaka 2019.

Related Articles

Back to top button