TIMU ya Simba imethibitisha kuachana na beki wake Mohamed Ouattara.
Mohamed Ouattara raia wa Ivory Coast alijiunga na Simba Julai 2022.
“Uongozi wa klabu unatangaza kutoendelea na mlinzi wa kati Mohamed Ouattara,” imesema Simba kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Huyo ni mchezaji wa pili Simba kutangaza kuachana naye leo baada ya Victor Akpan.