Simba, Yanga kuanzia nyumbani FA

DAR ES SALAAM: MABINGWA watetezi wa CRDB Federation Cup Yanga SC wamepangwa kucheza na Coastal Union katika hatua ya 32 bora ya miachuano hiyo.
Pia, Simba wao watacheza na TMA Stars ya championship, huku Azam FC watacheza na Mbeya City ambayo pia, iko Championship.
Tanzania Prisons itacheza dhidi ya Bigman FC, Kagera Sugar dhidi ya Namungo FC, Cosmopolitan dhidi ya KMC FC na Mbeya Kwanza dhidi ya Mambali Ushirikiano.
Nyingine, ni Polisi Tanzania dhidi ya Songea United FC, Kiluvya FC dhidi ya Pamba Jiji FC, Mtibwa Sugar dhidi ya Town Stars FC na JKT Tanzania dhidi ya Biashara United.
Girrafe Academy wamepangwa na Green Warrious FC, Tabora United dhidi ya Transt Camp, Mashujaa dhidi ya Geita Gold, Singida BS dhidi ya Leo Tena huku Fountain Gate wakipangwa dhidi Stand United.
Ratiba hiyo imetokana na droo iliyochezeshwa Leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)