
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu ukiwemo wa dabi ya timu za watoza kodi.
Katika dabi hiyo KMC itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Maafande wa JKT Tanzania itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Munungu Complex, Turiani Morogoro.
Kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa maafande wa Tanzania Prisons.