Filamu

‘Teaser’ ya Ngome ya Kifalme yazinduliwa leo

SEOUL: KAMPUNI ya utayarishaji filamu na tamthilia ya Disney+ imezindua kionjo (teaser) cha kwanza ya tamthilia mpya ya Korea Kusini ijulikanayo kwa jina la ‘The Remarried Empress’, ikiwashirikisha mastaa Shin Min-a, Ju Ji-hoon, Lee Jong-suk na Lee Se-young.

Teaser hiyo imezinduliwa leo Jumatano, Agosti 26, 2026, sambamba na mabango rasmi ya wahusika, huku Disney+ ikitangaza kuwa tamthilia hiyo itaanza kuoneshwa rasmi Novemba 4, 2026.

‘The Remarried Empress’ ni tamthilia ya kimapenzi inamulzea Navier jina linalotumiwa na Shin Min-a, ambaye ni malkia mwenye heshima wa Dola ya Mashariki.

Maisha yake yanaanza kubadilika baada ya mumewe, Mfalme Sovieshu, nafasi inayoigizwa na Ju Ji-hoon, kuvutiwa na Rashta nafasi inayochezwa na Lee Se-young. Hatimaye Sovieshu anamtaka Navier waachane ili aweze kumuoa Rashta.

Badala ya kukubali kudhalilishwa, Navier anaamua kukubali talaka hiyo lakini anaomba ruhusa ya kuolewa tena na Prince Heinrey, nafasi inayoigizwa na Lee Jong-suk kutoka Dola ya Magharibi.

Teaser mpya inaanza kwa kuonesha mandhari ya kifalme ya Dola ya Mashariki, kabla ya kumtambulisha Navier.

Katika sehemu nyingine, Sovieshu anaonekana akiahidi kumpenda Navier, lakini uhusiano wao unaanza kuvurugika baada ya kuwasili kwa Rashta.

Kuonekana kwa Prince Heinrey kunazidisha mvutano huo, huku akianza kuwa karibu na Navier na kuleta sura mpya katika mgogoro wa kifalme.

Disney+ imethibitisha kuwa ‘The Remarried Empress’ itaanza kuoneshwa Novemba 4, 2026. Tamthilia hiyo pia imepangwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Busan.

Related Articles

Back to top button