Filamu ya ‘TOXIC’ yaanza kwa kasi Box Office yapiga bilioni 7 kwa saa 3

NEW DELHI, INDIA: FILAMU mpya ya nyota wa India, Yash, ‘Toxic: A Fairy Tale for Grown-Ups’, imeanza kuoneshwa katika kumbi za sinema duniani leo Jumatano, Agosti 26, 2026, huku ikianza kwa kasi kubwa katika siku yake ya kwanza.
Filamu hiyo iliyoongozwa na Geetu Mohandas imetoka katika lugha kadhaa, ikiwemo Kannada, Hindi, Tamil, Telugu na Malayalam, huku ikiwa na nyota wengine kama Kiara Advani, Nayanthara, Huma Qureshi na Tara Sutaria.
Kwa mujibu wa taarifa ya Indian Express iliyochapishwa leo Agosti 26, majira ya saa 9.300 asubuhi ‘Toxic’ ilikuwa tayari imekusanya takribani ₹19.18 crore fedha za India ambazo ni sawa na bilioni 5.33 za Tanzania hii ni kwa mujibu wa takwimu za Sacnilk.
Baadaye, Hindustan Times iliripoti kuwa kufikia saa 5:00 asubuhi, filamu hiyo ilikuwa imefikia takribani ₹27.45 crore net nchini India, ambazo nis awa na bilioni 7 za Tanzania huku ikiwa na kiwango cha juu cha watazamaji katika maonesho ya asubuhi, hasa katika toleo la Kannada.
Licha ya mwanzo huo mzuri wa kibiashara, ‘Toxic’ imepokea maoni mchanganyiko kutoka kwa watazamaji na wakosoaji.
Baadhi ya watazamaji wamepongeza uigizaji wa Yash, mwonekano wa filamu na matukio ya mapigano, lakini wengine wameikosoa kwa upande wa maandishi, uhariri na urefu wa filamu.
Filamu hiyo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na kuwa filamu ya kwanza ya Yash kuingia kwenye sinema baada ya ‘KGF: Chapter 2’ ya mwaka 2022.




