Donald Trump, Hillary Clinton watoa rambirambi kifo cha mwanamuziki

NASHVILLE, MAREKANI : MWANAMUZIKI maarufu wa muziki wa country, mwandishi wa nyimbo na mwigizaji Dolly Parton, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Familia yake ilitangaza kifo chake, Agosti 25, 2026, huku taarifa zikieleza kuwa Parton alifariki akiwa Nashville, Tennessee, Marekani.

Parton alikuwa mmoja wa wasanii mashuhuri zaidi katika historia ya muziki wa country, akiwa na kazi iliyodumu kwa takribani miongo sita. Alijulikana kupitia nyimbo kubwa kama ‘Jolene,’ ‘9 to 5’ na ‘I Will Always Love You.’
Taarifa za awali kutoka kwa familia na vyombo vya habari zimeeleza kuwa alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, huku taarifa zaidi kuhusu afya yake zikifuatiliwa baada ya kifo chake.
Kifo cha Parton kimeibua majonzi makubwa duniani, huku mastaa, viongozi na mashabiki wakitoa salamu za rambirambi na kuelezea mchango wake katika muziki na jamii.
Kwa mujibu wa Reuters, miongoni mwa waliotoa heshima zao ni Donald Trump, Hillary Clinton, Jane Fonda, Vince Gill, Reba McEntire, Linda Ronstadt, Cyndi Lauper na Mick Jagger.
Reuters pia imeripoti kuwa mashabiki kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekusanyika na kuacha maua, mishumaa na ujumbe wa kumbukumbu katika maeneo yanayohusishwa na Parton, ikiwemo nyota yake kwenye Hollywood Walk of Fame.
Mbali na muziki, Parton alijulikana pia kwa shughuli zake za kijamii na kutoa msaada kwa watoto kupitia programu yake ya Imagination Library, pamoja na mchango wake katika elimu na tafiti za afya.
Kwa mujibu wa Reuters, Parton alikuwa ameuza zaidi ya rekodi milioni 100 duniani na alikuwa mshindi wa Grammy Awards 11, ikiwemo tuzo ya heshima ya Lifetime Achievement Award.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa katika muziki wa Marekani, huku dunia ya burudani ikiendelea kumuenzi kama mmoja wa wasanii walioacha alama kubwa katika muziki, filamu na shughuli za kibinadamu.




