Sara Ali Khan akiri kuwa na wivu

MUMBAI: MUIGIZAJI wa India, Sara Ali Khan amefichua kwamba aliwahi kumuonea wivu muigizaji mwenzake Alia Bhatt kwa namna alivyokuwa akiishi maisha ya kistaa.
Sara Khan ameendelea kueleza kwamba licha ya kutamani maisha ya muigizaji mwenzake huyo Alia Bhatt pia aliingiwa na wivu na Alia aliyefunga ndoa Ranbir Kapoor mnamo 2022 na mwaka huo huo akapata mtoto Raha na mwaka uliofuata 2023 akashinda Tuzo la Kitaifa kupitia filamu yake ya mwaka 2022 ya ‘Gangubai Kathiawadi’.
Akizungumza na NDTV Yuva, Sara amesema alihisi wivu zaidi Alia aliposhinda Tuzo la Kitaifa. Wakati huo, Sara Ali Khan alikuwa na fikra kwamba maisha ya Alia yalipangwa maana alikuwa na kila kitu alichokitaka akiwemo mtoto.
“Alia alipopata Tuzo ya Kitaifa, nilisema, ‘Mungu amepata, ana mtoto pia, maisha yake yamepangwa.’ Lakini sijui alipitia nini kupata hiyo mimi, kama muigizaji, nilimkosea sana utu.
“Mara nyingi tunapowaonea wivu watu wengine tunajisikia hivyo bila kujali chochote tunakuwa kama wehu tusiojua chochote. Tuna wivu kwa sababu tunaona tu mafanikio yao halafu tunayataka. Hatuoni kinachoendelea nyuma yake, hatuoni kamwe. Wivu ni upofu,” ameongeza.