Kwingineko

Manchester United yamtangaza Carlos Baleba, asaini hadi 2031

MANCHESTER: Klabu ya Manchester United imemtangaza rasmi kiungo wa kimataifa wa Cameroon, Carlos Baleba, kuwa mchezaji wake mpya baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Brighton & Hove Albion.

United ilitangaza usajili huo wa Baleba utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2031, pamoja na kipengele cha kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amewasili Manchester baada ya kuitumikia Brighton kwa misimu mitatu, ambapo alicheza jumla ya michezo 112 na kufunga mabao manne.

Taarifa za thamani ya uhamisho zinaonesha kuwa Manchester United imelipa takribani pauni milioni 65, huku ada hiyo ikifikia pauni milioni 70 kutokana na malipo ya ziada yanayohusishwa na mkataba huo.

Baada ya kukamilisha uhamisho huo, Baleba ameonesha furaha kubwa kwa kujiunga na Manchester United, akieleza kuwa ni hatua muhimu katika maisha yake ya soka.

Kiungo huyo wa Cameroon anatarajiwa kuongeza nguvu katika eneo la kiungo cha Manchester United, ambayo imekuwa ikifanya maboresho makubwa ya kikosi katika dirisha hili la usajili.

Baleba alijiunga na Brighton akitokea Lille mwaka 2023 na ndani ya muda mfupi akajijenga kuwa mmoja wa viungo muhimu wa klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya England.

Baleba alicheza michezo 31 ya Premier League, huku takwimu zake zikimuonyesha akiwa miongoni mwa viungo bora katika baadhi ya vipengele vya ukabaji na ushindi wa mipira ya pili.

Usajili wake unaifanya Manchester United kuendelea kuimarisha safu yake ya kiungo baada ya pia kumsajili Youri Tielemans na Andrey Santos katika dirisha hili la usajili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button