Ligi KuuNyumbani

Tano zamfuta kazi Robetinho

SIKU mbili baada ya klabu ya Simba kupata kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu hiyo imevunja mkataba na Kocha Mkuu Roberto Oliveira.

Taarifa ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula imesema vilevile klabu hiyo imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

“Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo(Robetinho),” imesema taarifa hiyo.

Simba imesema katika kipindi cha mpito kikosi cha Simba kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Kwa mujibu wa klabu hiyo tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Related Articles

Back to top button