EPL

Howe aachia ngazi Newcastle United

LONDON: Kocha Eddie Howe ametangaza kuondoka Newcastle United tangu achukue jukumu la kuinoa timu hiyo mwaka 2021.

Mtandao wa SkySports umefafanua kuwa maamuzi hayo ni baada ya majadiliano ya saa 48 baina ya uongozi wa Newcastle na Howe kuhusu uelekeo wa klabu na hatma yake.

Kinachotajwa kumuondoa Howe ni uongozi wa timu hiyo kushindwa kusimamia misimamo yake ya kuijenga na kuifikisha mbali timu, baada ya kuuzwa kwa Sandro Tonali na Anthony Gordon.

Kama haitoshi, nahodha Bruno Guimares anatajwa kutimkia Arsenal muda wowote kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Msimu uliopita, Newcastle pia ilimuuza Alexander Isak kwenda Liverpool kwa rekodi ya Pauni milioni 125.

Howe, 48 anaondoka akiwa miongoni mwa makocha bora kuinoa Newcastle kwani aliwapa Kombe la EFL mwaka 2025, lililokuwa kombe la kwanza kwa timu hiyo baada ya miaka 70.

Licha ya kutengeneza Newcastle yenye ushindani mkubwa lakini aliipeleka Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili mfululizo baada ya kumaliza tano bora Ligi Kuu England.

Howe, anaondoka zikiwa zimebaki siku 25 kabla ya mechi yao ya ufunguzi ya ligi dhidi ya Liverpool na inaelezwa Newcastle sasa inamtaka kocha wa Al Ahli, Matthias Jaissle, 38.

Wengine wanaotajwa kuwa kwenye orodha ya kufuatwa na mabosi wa timu hiyo kumrithi Howe ni Kieran McKenna na Antonio Conte.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button