Shalulile: Derby ya Kariakoo inanipa msisimko

DAR ES SALAAM: Mshambuliaji mpya wa Yanga, Peter Shalulile, amesema tayari anahesabu siku kuelekea Kariakoo Derby, akieleza kuwa kila anaposikia kuhusu pambano hilo la watani wa jadi kati ya Yanga na Simba hupata hisia kali za msisimko ‘Goosebumps’.
Nyota huyo, ambaye ametua Jangwani kwa matarajio makubwa ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Tanzania, alisema ukubwa wa derby hiyo umeanza kumgusa hata kabla hajavaa jezi katika mchezo huo.
“Ninaposikia kuhusu Derby ya Simba na Yanga, mwili wangu husisimka na nywele husimama. Tayari ninasubiri kwa hamu kubwa kuicheza mechi hiyo,” alisema Shalulile.
Kauli ya mshambuliaji huyo imeongeza hamasa kwa mashabiki wa Yanga ambao wanaamini uzoefu wake na uwezo wake wa kufunga mabao utakuwa silaha muhimu katika michezo mikubwa, hususan Kariakoo Derby inayovuta hisia za mamilioni ya mashabiki ndani na nje ya Tanzania.
Shalulile anajiunga na Yanga akiwa na rekodi ya mafanikio katika soka la Afrika Kusini, ambako alijijengea sifa kama mmoja wa wafungaji mahiri zaidi. Sasa macho ya wengi yataelekezwa kuona jinsi atakavyoanza maisha yake mapya akiwa na jezi ya kijani na njano.
Shalulile alisema rafiki yake anayecheza Tanzania alimwambia mechi ya Derby inahali kubwa mabyo huwezi kuizungumzia wakati wa maandalizi yake hadi siku ya mchezo. Kuwa Shalulile anatambua uzito wa Kariakoo Derby na shauku yake ya kushiriki pambano hilo imeongeza matarajio ya mashabiki wanaosubiri kumuona akivaana na watani wao wa jadi, Simba.




