Ligi Kuu

KMC: Azam waje waone, tumekaa pale!

DAR ES SALAAM: KOCHA Msaidizi wa KMC FC,  John Matambala amesema safari hii wanafuta uteja mbele ya wapinzani wao Azam FC, kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

KMC wanashuka dimbani kesho kutafuta pointi tatu muhimu dhidi ya Azam FC, Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Dar es Salaam.

Akizungumza kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho saa 10:00 jioni kocha huyo amesema msimu uliopita walipoteza alama sita mbele ya Azam FC, safari hii hawataki kuona matokeo hayo yanajirudia.

“Tunaangalia mechi ya mbele yetu dhidi ya Azam FC, wapinzani wetu wako vizuri na wana ubora, haitakuwa rahisi kwa sababu tumejipanga kutafuta pointi tatu mchezo wa kesho,” amesema kocha huyo.

Amesema wanaingia kwa nidhamu kubwa kwa kuwa wameshinda mechi iliyopita na Azam FC hawakupata pointi tatu na anaimani wataingia kivingine.

“Tumewaandaa wachezaji wetu kisaikolojia kwa ajili ya kukabiliana na Azam FC kesho, hatukubali kuwa wateja wao kwa mara ya tatu,” amesema Matambala

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button