Priscilla atamani kuwapa zawadi Nandy, Zuchu &Paula

DAR ES SALAAM:MPENZI wa Msanii wa Bongo Fleva nchini Juma Mussa ‘Jux’ kutokea nchini Nigeria Priscilla Ojo amesema anatamani kuwapa zawadi wasanii wa hapa nchini Faustina Mfinanga ‘Nandy’, Zuhura Othuman ‘Zuchu’ na Paula Kajala zawadi ya ubalozi wa taulo za wanawake za Ora.
Akizungumza Dar es Salaam leo wakati alipotangazwa kuwa balozi wa taulo hizo Priscilla amesema hao ndio wasanii wa kike anaowakubali na wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki.
“Nashukuru watanzania kwa kunipa ubalozi naamini nitakuwa balozi mzuri na zitajulikana kimataifa, wasanii niliowataja nawapenda na ndio sababu nimewachagua kuwapa zawadi ya taulo “amesema.
Kwa upande wake Zamaradi Mketema ambaye ni mshiriki kibiashara wa taulo za Ora amesema kuwa watatoa elimu kwa Wanafunzi kuhusiana na hedhi na umuhimu wa kutumia katika afya.
“Wanafunzi wa kike tutawapatia elimu kuhusiana na matumizi ya taulo wajue kuwa kupata hedhi sio dhambi wala sio jambo la aibu na kushangaza bali ni jambo la kujivunia.
“Kwanza kabisa wajue kupata hedhi ni afya na kufurahia kuwa mwanamke sio kuchekwa na kufedheheshwa bali kuwa jasiri kwa kilichokupata na tutawapatia taulo hizo ziwasaidie kuendelea na masomo kwa uhuru zaidi,”alisema.