Mastaa

Anayemtishia kifo Salman Khan ni mgonjwa wa akili

MUMBAI: MWANAUME anayedaiwa kutoa tishio la kifo kwa muigizaji Salman Khan, amefuatiliwa hadi kijiji kimoja katika wilaya ya Vadodara huko Gujarat na kugundulika kuwa na matatizo ya kiakili, polisi wamesema mapema leo Jumanne Aprili 15, 2025.

Polisi wa Mumbai wametoa notisi kwa mwanamme mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa kijiji cha Waghodia taluka, kujisalimisha.

Nambari ya usaidizi ya WhatsApp ya Polisi wa Trafiki ya Mumbai ilipokea ujumbe siku ya Jumapili iliyopita ambapo mtumaji huyo alitishia kulipua gari la Salman Khan kwa bomu na kumvamia mlinzi wa Y-Plus kwa kuingia kwenye makazi yake.

Baadaye, polisi wa Worli huko Mumbai walisajili kesi dhidi ya mtu ambaye hakujulikana wakati huo chini ya kifungu cha 351 cha Bharatiya Nyaya Sanhita na kuimarisha usalama nje ya makazi ya Khan katika eneo la Bandra.

Kufuatia uchunguzi, polisi wa Mumbai waligundua kuwa tishio hilo lilitumwa na mtu anayeishi Waghodia taluka ya Vadodara, Msimamizi wa Polisi wa wilaya Rohan Anand aliwaambia waandishi wa habari.

“Kikosi cha polisi wa Mumbai, wakiandamana na polisi wa Waghodia, walifika nyumbani kwa mshukiwa katika kijiji cha Waghodia jana Jumatatu. Hata hivyo, ilibainika kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye alikuwa ametuma ujumbe huo, hana akili timamu na matibabu yake pia yanaendelea,” Anand amesema.

Mnamo Aprili mwaka jana, watu wawili wanaotumia pikipiki walifyatua risasi nne nje ya makazi ya Khan kwenye Jumba la Galaxy Apartments katika eneo la Bandra huko Mumbai.

Hapo awali Khan alikabiliwa na vitisho kutoka kwa genge la Lawrence Bishnoi, ambalo lilimuonya juu ya athari ikiwa hataomba msamaha kwa jamii ya Bishnoi kwa madai ya mauaji ya blackbuck. Kufuatia vitisho hivi, polisi wa Mumbai walimpa ulinzi wa Y-Plus.

Wiki kadhaa baada ya kisa cha kurusha risasi mwaka jana, Polisi wa Navi Mumbai walidai kugundua njama ya genge la Bishnoi kumuua Khan aliposafiri kwenda shambani kwake Panvel karibu na Mumbai.

Related Articles

Back to top button