Mastaa

Irene Uwoya azua gumzo mtandaoni kwa picha za mapenzi

DAR ES SALAAM:MSANII maarufu wa filamu nchini, Irene Uwoya, anayefahamika pia kama Mama Mchungaji, ameibua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha zinazomuonesha akiwa katika mapozi ya kimapenzi na mwanaume, huku wote wakiwa wamevalia mavazi yanayoashiria tukio maalum.

Katika picha hizo, Uwoya na mkaka huyo wanaonekana wakiwa kwenye mazingira ya kimahaba, jambo lililopelekea mashabiki wake kuanza kujiuliza maswali mengi, je, ni kweli amefunga ndoa au anatarajia kufunga?

Wengine wameonekana kumpongeza, wakiamini huenda amepata mpenzi mpya, huku baadhi wakihisi kwamba huenda ni sehemu ya tamthilia mpya anayoigiza.

Hadi sasa Uwoya mwenyewe hajatoa ufafanuzi wowote kuhusu picha hizo, jambo linaloacha mashabiki wake kwenye sintofahamu.

Related Articles

Back to top button