Muziki

Oshibibi ya Gasper yatikisa Afrika Mashariki

MAREKANI: MSANII wa kizazi kipya anayeishi Marekani, Gasper Welongo, ameendelea kufanya vizuri kwenye anga la muziki baada ya wimbo wake mpya Oshibibi kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Gasper, ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Marekani, amesema mafanikio ya wimbo huo yamezidi matarajio yake kutokana na idadi kubwa ya watazamaji na wasikilizaji wanaoendelea kuufuatilia kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali.

Akizungumza na Spoti Leo, msanii huyo alisema Oshibibi imekuwa daraja muhimu kwake kurejea kwa nguvu kwenye soko la muziki wa nyumbani pamoja na kuongeza mashabiki wapya ndani na nje ya Tanzania.

“Oshibibi imenifungulia njia kubwa zaidi huko nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Nimepata namba kubwa sana kwenye chaneli yangu ya YouTube, na naamini mashabiki wanaendelea kunipa sapoti ili kwa pamoja tuufikishe muziki wetu mbali zaidi,” amesema Gasper.

Mashabiki wengi wameonekana kuvutiwa na ladha mpya ya muziki aliyoileta kupitia wimbo huo, jambo ambalo limechangia kuendelea kupaa kwa jina lake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Related Articles

Back to top button