Muziki

Diamond, Nandy kuwakilisha tuzo za AEAUSA

MSANII wa muziki wa , Bongo fleva nchini Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ametajwa kuwania tuzo za AEAUSA katika kipengele cha ‘Best Female Artist’ akishindana na wasanii kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Simi, Ayra, Tems, Makhadzi, Tyla, Aya Nakamuru na Niniola.

Huku msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akichuana na mastaa kutoka Nigeria katika tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) zinazotarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu.

Hayo ni baada ya AEAUSA kutoa orodha ya wasanii na vingengele watakavyowania katika tuzo hizo, ambapo katika kipengele cha ‘Artist of the Year’ Diamond atatoana jasho na mastaa kama Burna Boy, Davido, Yemi, Ayra, Asake, Rema, Wizkid, Adekunle na msanii kutoka Afrika Kusini, Tyla.

Mbali na kutajwa katika kipengele hicho Diamond pia yupo kwenye kipengele cha ‘Best Male Artist’ akichuana na wasanii kama Davido, Harmonize, Burna Boy, Wizkid, Olamide, Rema, Kizz Daniel, Black sheriff na Fally Ipupa.

Related Articles

Back to top button