Nyumbani
Nkane nje wiki 6

WINGA wa klabu ya Yanga Dennis Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya vipimo kuonyesha amevunjika mfupa mdogo unaosababisha nyonga kujikunja.
Kwa mujibu taarifa ya daktari wa Yanga, Moses Etutu, Nkane atakuwa na vipindi viwili vya kuuguza majeraha yake hadi hapo atakaporejea rasmi uwanjani.
“Atakaa nje kwa wiki nne halafu wiki mbili za mwisho ataanza mazoezi mepesi ambayo tutakuwa tunamfuatilia tujue maendeleo yake,” alisema Dokta Moses.
Nkane aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Disemba 20 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.