Nyumbani

Ishu ya Saido kutua Coastal imekaa hivi!..

TANGA: WAKATI kiungo mshambuliaji wa Simba, Said Ntibanzonkiza akihusishwa kusajiliwa Coastal Union, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi wamekutana na meneja wa mchezaji huyo kwa ajili ya mazungumzo.

Coastal Union anahusishwa kufanya mazungumzo Ntibazonkiza na Djuma Shabaani li kuimarisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ambapo wanaenda kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na Spotileo, Ofisa Habari wa Coastal Union, Abass Elsabri amesema ni mapema kuzungumzia juu ya usajili wa nyota hao kwa sababu Meneja wa Ntibanzokiza amefika mezani kwa viongozi hao kwa ajili ya kutaka kufanya mazungumzo.

Amesema kipindi cha usajili kuna wachezaji ambao wanahusishwa nao lakini wao wanaangalia maboreshao na wachezaji watakaowasajili na kwenda kusaidia timu hiyo katika michuano ya kimataifa.

“Ni kweli Meneja wa Ntibanzonkiza alikuja kukutana na viongozi lakini hakuweka wazi juu ya hatma yao, suala la usajili linaendelea na ukizingatia dirisha limefunguliwa na tunasajili wachezaji wenye uzoefu wa kusaidia timu kufanya vizuri kimataifa,” amesema Abass.

Amesisitiza kuwa hawatafanya usajili kwa kufuata majina makubwa bali wanahitaji kuleta watu wenye uzoefu na kusaidia timu hiyo kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara.

Related Articles

Back to top button