Ligi KuuNyumbani

Singida BS kurejesha makali yake leo?

LIGI Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Dar es Salaam na Kagera.

Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ugenini Singida Big Stars itakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Singida Big Stars ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 6 wakati Kagera Sugar inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 7.

Katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, majirani wawili KMC na Azam zitakutana katika uwanja wa Uhuru huku KMC ikiwa mwenyeji.

Azam inashika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 6 wakati KMC ipo nafasi ya 6 ikwa na pointi 10 baada ya michezo 7.

Katika mchezo wa mwisho wa ligi kai ya timu hizo mbili Mei 7, 2022 Azam iliibuka mshindi dhidi ya KMC kwa mabao 2-1.

Related Articles

Back to top button