Mzee Samatta: Mbwana rudi timu ya Taifa, mimi nilifukuzwa kabisa
DAR ES SALAAM: MCHEZAJI bora wa kwanza wa zamani nchini Ally Samatta amemshauri mtoto wake Mbwana Samatta kurudi kuitumikia timu ya Taifa huku akifananisha namna yeye alivyofukuzwa kabisa katika timu ya taifa mwaka 1964 kutokana na utovu wa nidhamu.
Anasema mwaka huo alikuwa mchezaji tegemeo wa timu ya taifa na timu ya mtaani kwao aliamua Kwenda kucheza kwenye fainali ya mashindano ya Kombe la Kamanda mwaka huo wa 1964 na akafanikiwa kufunga mabao matatu yote na wakafanikiwa kubeba kombe lakini aliporudi kambini akafukuzwa.
“Mwaka 1994 nilikuwa mchezaji tegemeo wat imu ya Taifa lakini timu yangu ya mtaani kwetu ilikuwa inamchezo muhimu mno katika mashindano ya kombe la Kamanda kipindi hicho nilitakiwa kuwa kambi ya taifa stars lakini nilikwenda kucheza kombe la Kamanda na nikafunga magoli matatu yote tukashinda lakini niliporudi kambini taifa stars nilifukuzwa kwa utovu wa nidhamu.
“Lakini kipindi hicho mwalimu wat imu alikuwa mzungu Mserbia aliporudi hakuniona akauliza yuko wapi mchezaji wangu wakamjibu tumemfukuza akawaambia namtaka yule ni mchezaji bora na muhimu kwa timu kocha alinirudisha nikarudi timu ya taifa tukafanya vizuri sana,” ameeleza mzee Samatta akifananisha changamoto alizopata kipindi alipokuwa akicheza timu ya taifa na namna mwanae Mbwana samatta anachokutana nacho kwa mashabiki.
Mzee Samatta amesema kwa sasa Mbwana anafanya vizuri na timu yake ya PAOK Thessaloniki FC ya nchini Ugiriki na amekuwa na mchango mzuri hadi hapo ilipofikia hivyo anakila sababu ya kuendelea kuisaidia timu ya taifa.
“Mbwana anamchango mkubwa kwa timu yake ya huko Ugiriki alafu aseme anajiuzulu timu ya taifa nani atakubali mashabiki wanaompenda hawawezi kukubali hata viongozi hawawezi kukubali nami sitakubali arudi acheze timu inamuhitaji anamchango mkubwa kwa taifa,” alimaliza mzee Samatta.