Ligi KuuNyumbani

Aziz Ki mchezaji bora Oktoba

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) imemchagua kiungo mshambuliaji wa Yanga Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Taarifa ya TPLB imesema Ki amewashinda Moses Phiri wa Simba na Max Nzengeli wa Yanga kwenye mchakato wa Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Ki alifunga mabao manne katika dakika 278 za michezo minne aliyochezea timu yake mwezi huo.

Pia kamati hiyo imemchagua Roberto Oliveira wa Simba kuwa kocha bora wa ligi hiyo Oktoba baada ya Simba kushinda michezo mitatu mwezi huo.

Tuzo ya Meneja bora wa uwanja imekwenda kwa Malule Omar wa uwanja wa Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button