Kwingineko

‘Niliiona nyumba yangu ikiteketea kwa moto kwenye runinga’

LOS ANGELES: MWANAMITINDO, Mwimbaji, Muigizaji na Dj maarufu nchini Marekani anayetokea Los Angeles, Paris Hilton amesema alihisi moyo wake kupasuka vipande zaidi ya milioni baada ya kushuhudia kwenye runinga nyumba yake ikiteketea kwa moto.

Licha ya kupoteza nyumba hiyo iliyokuwa na thamani ya dola milioni 8.4, DJ huyo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri ameshukuru kuwa salama yeye pamoja na mume wake, Carter Reum na watoto wao wawili.

Katika chapisho lake kwenye ukurasa wake wa Instagram, aliandika: “Nimesimama hapa katika iliyokuwa nyumba yetu, na huzuni ya moyo haiwezi kuelezeka,

“Nilipoona habari hiyo kwa mara ya kwanza, nilishtuka kabisa – sikuamini. Lakini sasa, nikisimama hapa na kuiona kwa macho yangu mwenyewe, ninahisi kama moyo wangu umevunjika vipande milioni.”

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 43 ambaye pia ni mjukuu wa Conrad Hilton, mwanzilishi wa Hilton Hotels alinunua nyumba hiyo kwa dola milioni 8.4 mwaka 2021 alichapisha video inayoonyesha mabaki ya nyumba yake yaliyokuwa yakifuka moshi na kuongeza:

“Nyumba hii haikuwa mahali pa kuishi tu bali ni mahali tulipoota, tukacheka, na kuunda kumbukumbu nzuri zaidi kama familia.

“Ni nyumba ambayo ilitengeneza sanaa ambayo nitaithamini milele, ambapo upendo na maisha vilijaa kila kona. Kuiona ikipunguzwa na kuwa majivu inaumiza kupita maelezo.

“Kinachovunja moyo wangu zaidi ni kujua kwamba hii sio hadithi yangu tu. Watu wengi sana wamepoteza kila kitu. Sio tu kuta na paa – ni kumbukumbu ambazo zilifanya nyumba hizo kuwa nyumba. Ni picha, kumbukumbu, vipande visivyoweza kubadilishwa vya maisha yetu.”

Paris aliendelea kuongeza: “Na bado, katika maumivu haya, najua nina bahati sana. Wapendwa wangu, watoto wangu wachanga, na wanyama wangu wa kipenzi wako salama. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi, na ninashukuru kwa kila kitu nilicho nacho.

“Na zaidi ya kuwashukuru wazima moto wote, wahudumu wa kwanza na watu waliojitolea kuhatarisha maisha yao ili kupambana na moto huu.”

Paris pia aliwashukuru mashabiki wake wote kwa kumtumia salamu za pole, kumuombea huku akiapa kujijenga upya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button