Man City Vs Spurs mechi ya kisasi

LONDON, ENGLAND: Tottenham Hotspurs itawakaribisha wababe wa wa Ligi kuu ya England Manchester City katika raundi ya nne ya kombe la Carabao, mchezo utakaochezwa katika dimba la Nyumbani la Tottenham Hotspur jijini London.
Mchezo huu unachukuliwa kama wa kisasi kwani ni marudio ya fainali ya Kombe hilo la Carabao msimu 2020/21 tofauti tu ni mara hii utachezwa katika raundi ya nne.
Katika fainali hiyo Spurs ilichapwa bao 1-0 na kikosi cha Guardiola kwenye Uwanja wa Wembley goli la Aymeric Laporte aliyefunga kwa kichwa. Mchezo huo utapigwa Oktoba 28 mwaka huu.
Michezo mingine ya raundi ya nne ya Carabao cup
Brentford vs Sheffield Wednesday
Southampton vs Stoke City
AFC Wimbledon/Newcastle vs Chelsea
Man United vs Leicester
Brighton vs Liverpool
Preston vs Arsenal
Aston Villa vs Crystal Palace