Van Nistelrooy, Leicester waachana

LONDON, Klabu ya Leicester City iliyoshuka Daraja msimu uliopita imetangaza kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Ruud van Nistelrooy baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kukubali kusitisha mkataba wake kama kocha wa klabu hiyo
Van Nistelrooy alichukua mikoba ya kuinoa Leicester mwezi Novemba mwaka jana kwa mkataba uliokuwa utamatike mwezi Juni mwaka 2027, lakini hakuweza kuisaidia klabu hiyo kuepuka kushuka daraja baada ya kumaliza katika nafasi ya 18 kwenye Ligi na sasa Leicester imesema inatafuta mbadala wake.
Klabu hiyo ilimshukuru Van Nistelrooy kwa kujitolea na bidi yake wakati wote wakati nyota huyo wa zamani wa Manchester United akiitakia timu kila la Kheri. Van Nistelrooy mwenye umri wa miaka 48 amewahi kuifundisha PSV Eindhoven ya Uholanzi kabla ya kuwa kocha wa muda wa United.
Leicester wanakabiliwa na uwezekano wa kukatwa pointi kwenye ligi ya Champiomship baada ya kuwa chini ya uchunguzi kwa ukiukaji wa sheria za kifedha.