Nick Cannon afichua kilichomuondoa katika ndoa na Mariah Carey

NEWYORK:MCHEKESHAJI wa kimarekani, Nick Cannon amekiri kwamba alipata shida kumtambulisha aliyekuwa mke wake Mariah Carey wakati wa ndoa yao iliyodumu kati ya mwaka 2008 hadi 2016 kutokana na kuzidiwa umri na mke wake huyo.
Nick mwenye miaka 43 na Maria Carey mwenye miaka 55 walidumi katika ndoa kwa miaka nane tu na sasa wanalea watoto wao mapacha Moroccan na Monroe wenye miaka 11.
Wakati alipokuwa akihojiwa katika podicasti ya ‘Ray Daniels Presents’, Nick alieleza kwamba: “Kwa kweli siku ile sikujali sana ulimwengu ulifikiria nini kwa sababu mtazamo ndivyo ulivyo. Watu watakupenda siku moja, watakuchukia siku inayofuata,
“Ningeweza kujali kidogo kuhusu hilo Lakini nikaingiwa na shinikizo la, ‘Mimi ni nani?’ … Niliingia katika ndoa nikiwa katika miaka yangu 20, unajua ninachomaanisha? Tena nilimuoa staa mkubwa duniani aliyekuwa mkubwa sana zaidi yangu kisanii yeye alikuwa zaidi.
“Ana miliki vitu vingi vikiweo visiwa nilikwa nikilala hadi saa sita mchana nikiamka naletewa nyama kwenye sinia. Usiku nilikuwa nikilala nikifikiria, Je, hivi ndivyo nilivyo? Je, mimi ni mwanaume wa Mariah? Je, ndivyo maisha yangu yanavyopaswa kuwa? Najua hakuna ubaya wowote, lakini nilikuwa nikifikiria hivyo.”
Nick aliendelea kukiri kwamba upande wa familia nao ulikuwa na changamoto zake lakini pia hali ilizidi kuwa ngumu kwake baada ya kupata mapacha: “Nimebeba mkoba, mfuko wa diaper na, unajua, kuna sehemu nilikuwa nasimama kwenye kona kumsubiri mamaa akazungumze na watu wake anastahili hilo.
“Ninaamini anahitaji kuwa na mtu kama huyo. Mimi sifananii na huyo jamaa.” Alisema Nick bila kufafanua jamaa anayemwelezea hapo.
Hapo awali Mariah Carey alifunguka kuhusu ndoa hiyo katika kumbukumbu yake ‘The Meaning of Mariah Carey’ na kusisitiza kuwa walikuwa wazuri pamoja lakini ubinafsi uliingilia uhusiano wao.
Aliandika hivi: “Alikuwa mtu mzuri. Alikuwa na imani. Alikuwa na tamaa ya kujua mambo. Alikuwa kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu, kwa hivyo alielewa mambo ya kwenye tasnia ya burudani. Alinitilia maanani muda mwingi.
“Kusema kweli, Nick na mimi nadhani tungeweza kusuluhisha kati yetu sisi wawili, lakini ubinafsi na hisia zisizoelezeka zikafanya hali iwe ngumu kati yetu. Sote wawili tulitaka kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa kwa familia yetu. Tumekubaliana kuwa familia kila wakati, na tunaifanya hali hiyo ifanye kazi.”