Mastaa

Prezzo ajutia matumizi ya madawa ya kulevya

MSANII wa Muziki wa Hip-Hop kutokea nchini Kenya Jackson Ngechu, ‘Prezzo’ ameelezea majuto na mateso aliyoyapata kwa matumizi ya madawa ya kulevya na wanawake kwa umaarufu wake.

Prezzo amesimulia jinsi umaarufu ulivyoathiri maisha yake na kusema kuwa ndio sababu ya yeye kupanda na kushuka kimaisha na kutoa somo kwa watu maarufu kama yeye.

“Pamoja na umaarufu huja na mambo mengi, kupanda na kushuka, usumbufu, wanawake, dawa za kulevya. Sitasema kwamba sijawahi kutumia madawa ya kulevya.

“Mimi huvuta bangi mara kwa mara na dawa za kulevya. Nilikuwa nikitengeneza dawa hiyo, lakini kadiri muda ulivyosonga, nilipata madhara. Nilishawahi kutumia dawa za kulevya lakini jambo moja ninalomshukuru Mungu ni kwamba sijawahi kwenda kwenye kituo cha kurekebisha tabia na hiyo ni kwa sababu nina mawazo madhubuti”,amesema Prezzo.

Pia ameongeza kuwa Moja ya vitu vilivyomfanya atumie zaidi dawa za kulevya ni msongo wa mawazo baada ya kuachana na mke wake anayejulikama kama Diasy Kiplagat mwaka 2012.

Diasy alipowasilisha kesi ya talaka mwaka wa 2012, alimshutumu rapa huyo kwa kutumia dawa za kulevya, ujeuri na uzinzi.

Related Articles

Back to top button