Africa

Ni vita Raja vs Al Ahly CAF

BAADA ya wekundu wa Msimbazi, Simba kuondolewa na Wydad AC katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti, mechi nyingine tatu za hatua hiyo zinapigwa leo.

Raja Casablanca itakuwa uwanja wa nyumbani ikitaka kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahly kwa mabao 2-0.

Nayo Mamelodi Sundowns ambayo ilishinda mchezo wa kwanza jijini Algiers, Algeria kwa mabao 4-1 itaikaribisha CR Belouizdad kwenye uwanja wa Loftus Versfeld jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Katika mchezo mwingine JS Kabylie itakuwa ugenini kuikabili Esperance.

Related Articles

Back to top button