AfricaKusini Mwa Afrika
Twiga Stars karata ya tatu COSAFA

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake(Twiga Stars) leo itashuke dimbani katika mchezo wa tatu wa ubingwa wa Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika(COSAFA) kwa wanawake dhidi ya Malawi.
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Wolfson uliopo nje kidogo ya jiji la Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Twiga Stars iliyopo kundi C ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Comoros katika mchezo wa kwanza kabla ya kutoka suluhu na Botwana katika mchezo wa pili.
Mchezo mwingine wa kundi hilo leo ni kati ya Comoros na Botswana.