Africa

Ramovic aahidi raha

ALGERIA:KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kikosi chake kipo tayari kukabiliana na MC Alger katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kesho.

Yanga watakuwa ugenini katika mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa 5 Juillet kuanzia saa 4:00 usiku.

Ramovic amesema wanaenda kucheza na timu ngumu, ina wachezaji bora na kocha mzoefu lakini wana kikosi chenye wachezaji bora sana , anaamini itakuwa mechi nzuri yenye kuvutia.

“Yanga wana historia kwenye uwanja tutakaotumia kesho, walipoteza mchezo wa fainali hapa kwa kanuni lakini naamini walishinda mioyo ya wapenda mpira hapa Algeria,  kesho ni siku nyingine na tutakuja na nguvu nyingine ya kushinda mchezo.

Tuko kwenye presha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza , lakini imetupa nguvu ya kujiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho,  tumekuja mapema kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa, hatuwezi kuoanga matokeo ya mwisho yatakavyokuwa lakini tunawaza kupanga jinsi tutakavyocheza ili kupata matokeo mazuri,” amesema.

Ramovic amesema sio vizuri kucheza mechi bila mashabiki, anapenda kuiona timu yake ikicheza mbele ya mashabiki wengi, kesho watawakosa hivyo wana jukumu la kupambana kuwapa furaha mashabiki wao watakaokuwa Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button