Africa

Yanga vs Mamelodi mzunguko bure

MASHABIKI watakaoingia uwanja wa Benjamin Mkapa eneo la mzunguko wakati wa mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns hawalipa kiingilio.

Mchezo huo utafanyika Machi 30 wakati marudiano ni Aprili 5, Afrika Kusini.

Akizungumza Dar es Salaam leo Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema uongozi wa klabu hiyo umepunguza kiingilio na kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha mashabiki wengi wanakwenda uwanjani.

“Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa basi tunawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi,” amesema Kamwe.

Viingilio katika majukwaa mengine ni kama ifuatavyo:
𝐕𝐈𝐏 𝐂 𝟏𝟎,𝟎𝟎𝟎/-
𝐕𝐈𝐏 𝐁 𝟐𝟎,𝟎𝟎𝟎/-
𝐕𝐈𝐏 𝐀 𝟑𝟎,𝟎𝟎𝟎/-

Kamwe amesema uongozi wa Yanga pia umekubaliana kuweka mkakati wa kupeleka mashabiki Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano.

“Kama tulivyofanya wakati wa mchezo wetu wa nusu fainali CAFCC dhidi ya Marumo, ‘𝐓𝐰𝐞𝐧𝐳𝐞𝐭𝐮 𝐤𝐰𝐚 𝐌𝐚𝐝𝐢𝐧𝐚’ (kwao kama kwetu) season 2 inaanza,” amesema.

Kwa mujibu wa Kamwe gharama ya usafiri wa kwenda Afrika Kusini na kurudi kwa njia ya basi ni shs Laki Sita.

Related Articles

Back to top button