Tetesi

Newcastle yamtupia macho Barella

TIMU ya Newcastle United ‘The Magpies’ inatarajiwa kutuma ombi la kumsajili kiungo wa Inter Milan, Nicolo Barella.

Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England ina lengo la usajili viungo wawili msimu huu wa majira ya joto na Barella amekuwa kwenye rada za ‘The Magpies’.

Wamiliki wa Newcastle kampuni ya Saudi Arabia, Public Investment Fund, wapo tayari kumuunga mkono Kocha Mkuu Eddie Howe katika dirisha la usajili kwa kuweka bajeti kubwa ya uhamisho ili kufanikisha kusajili wachezaji kama Barella.

‘The Magpies’ wapo tayari kuishawishi Inter dili la pauni milioni 50 sawa na shilingi bilioni 147.7 lakini itaangaliwa iwapo kiasi hicho kitatosha kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26.

Hata hivyo, habari nyingine kutoka Italia zinasema makubaliano ya kumsajili Barella hayataweza kufikiwa hivi karibuni.

Inaeleweka kwamba kuwa Barella ana furaha Nerazzurri na habari zinasema itachukua hatua maalumu kumshawishi kuondoka katika klabu hiyo.

Related Articles

Back to top button