Real Madrid: Rodrygo hauzwi
TETESI za usajili zinasema Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu England vinavyohusudu Rodrygo Silva de Goe maarufu Rodrygo kujiunga na navyo. Arsenal na Manchester City pia zina nia kumsajili lakini Real Madrid kwa sasa haina nia kumuuza fowadi huyo mbrazil . (SPORT – Spain)
Liverpool ipo tayari kushindana na Real Madrid na Chelsea kumsajili beki wa kati wa Lille Leny Yoro, ambaye anaweza kugharimu pauni mil 51. (MARCA – Spain)
Arsenal imemjumuisha mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak kwenye orodha yake ya machaguo ya usajili wakati wa dirisha la uhamisho majira yajayo ya kiangazi.
Mchezaji mwenzake na Isak toka Sweden, Viktor Gyokeres, pia ni mlengwa wa usajili The Gunners. (Football Insider)
Manchester City inaweza kukaribisha ofa za vilabu mbalimbali kumsajili Jack Grealish majira yajayo ya kiangazi wakati ikisaka fedha kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya. (HITC)