Mke wa Bushoke amwagia sifa mumewe

DAR ES SALAAM: MKE wa msanii wa Bongo Fleva, Luta Bushoke maarufu kama Bushoke, Julieth Zawede, amempongeza kwa upendo mkubwa mume wake kupitia ujumbe maalum wa kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Julieth, mwenye asili ya Uganda na ambaye ameishi nchini Marekani kwa miaka mingi, amesema Bushoke ni mwanaume wa kipekee mwenye moyo wa upendo na baraka kwa kila anayepata nafasi ya kumfahamu.
Katika ujumbe wake, alimshukuru mume wake kwa furaha na upendo anaouleta katika maisha ya watu wanaomzunguka, huku akimtakia afya njema, mafanikio makubwa na baraka tele anapoanza mwaka mpya wa maisha yake.
Kwa upande wake, Bushoke hakusita kumshukuru mkewe kwa ujumbe huo wa kugusa hisia, akionesha kuthamini upendo na maneno mazuri aliyomwandikia katika siku yake maalum.
Bushoke na Julieth walifunga ndoa mwishoni mwa mwaka 2025 nchini Marekani, ambako wanaishi kwa sasa.
Mbali na Bushoke kujulikana kupitia muziki wa Bongo Fleva, Julieth pia aliwahi kujihusisha na muziki, huku akiwa mfanyabiashara na mwanaharakati anayejishughulisha na shughuli za kusaidia jamii.




