Nyavu

Magereza yaanza kwa kishindo wavu taifa

DAR ES SALAAM: TIMU ya Magereza imeanza kampeni zake katika mashindano ya Mpira wa Wavu Tanzania (TVNL) 2026 kwa ushindi wa kishindo baada ya kuichapa Bandari kwa seti 3-0.

Magereza ilionesha ubora wake katika mchezo huo na kutawala vipindi vyote, hivyo kuondoka na ushindi muhimu katika mbio za kuwania taji la msimu huu.

Mashindano ya wavu 2026 yamewakutanisha jumla ya timu 24, ambapo timu 14 zinashiriki upande wa wanaume huku timu 10 zikishindana upande wa wanawake.

Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF), Shukuru Said, amesema ushindani katika mashindano ya mwaka huu umekuwa mkubwa, huku kila timu ikionesha kiwango kizuri na dhamira ya kufanya vizuri.

Shukuru amesema anatarajia ushindani kuendelea kuongezeka zaidi katika raundi ya pili na kuelekea hatua za fainali, jambo litakalowapa mashabiki mechi zenye kuvutia na kuongeza chachu ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa wavu nchini.

Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Agosti 3 na itahitimishwa Agosti 10, mwaka huu.

 

Related Articles

Back to top button