Ligi Kuu

Azam FC yatangaza jezi zake za msimu mpya

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC imetangaza jezi zake mpya za nyumbani za msimu ujao, zikiwa na muundo wa kisasa unaolenga kuunganisha utambulisho wa timu, ubunifu na mahitaji ya mashabiki wake.

Huo ni utaratibu wa kawaida wa kila msimu timu ikionesha utayari wa kuanza msimu mpya. Jezi hizo zina rangi nyeupe na bluu kidogo zikiwa ndani ya rangi zao za siku zote.

Wakati ikiwasogeza mashabiki wake karibu kwa jezi mpya, Azam FC inaendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa kambini nchini Rwanda.

Timu hiyo ipo Rwanda kwa ajili ya kuweka sawa mipango yake ya kiufundi, kuongeza kiwango cha utimamu wa wachezaji na kujenga muunganiko wa kikosi kabla ya msimu kuanza.

Benchi la ufundi la Azam FC linatumia kipindi hicho kufanya tathmini ya wachezaji, kuboresha mifumo ya uchezaji na kuwapa nafasi wachezaji wapya kuzoeana na wenzao ili kuingia msimu wakiwa tayari.

Mbali na maandalizi ya uwanjani, Azam FC pia imeendelea kuimarisha upande wa kibiashara kupitia bidhaa rasmi za klabu, hatua inayolenga kuongeza ushiriki wa mashabiki na kukuza thamani ya chapa ya timu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button